Mahakama ya Tanzania

Mahakama ya Tanzania ni mfumo mzima wa mahakama unaotafsiri na kutumia sheria nchini Tanzania.

Mpaka sasa mahakama inafuata misingi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 [1]. Katika katiba ya Tanzania mahakimu pamoja na majaji hutegemewa na serikali na wapo chini ya sheria na katiba.

Nchi ina mifumo ya mamlaka miwili ambapo kuna muundo wa mahakama unaowajibika kwa Tanzania Bara na mwingine kwa Zanzibar[2].

Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano ilianzishwa mwaka 1979 kama chombo cha mwisho cha mahakama cha rufaa chenye mamlaka katika muungano mzima.

  1. https://www.constituteproject.org/constitution/Tanzania_1995.pdf?lang=en
  2. Bierwagen, Rainer Michael; Peter, Chris Maina (1989-04). "Administration of Justice in Tanzania and Zanzibar: A Comparison of Two Judicial Systems in one Country". International & Comparative Law Quarterly (kwa Kiingereza). 38 (2): 395–412. doi:10.1093/iclqaj/38.2.395. ISSN 1471-6895. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search